Kwa mujibu wa gazeti la Standard linalochapishwa Kenya toleo la Ijumaa Agosti 3, Mkuu wa Kenya Reinsurance Jadiah Mwania amesema kati ya walioteuliwa ni Maulamaa wa Kiislamu na wataalamu wa Qur'ani ili kutoa maelekezo kuhusu bima ya Kiislamu ya Takaful.
‘Bodi ya Sheria za Kiislamu itasaidia Kenya Reinsurance kushirikiana na mashirika ya bima yanayotoa huduma za bima ya Kiislamu nchini Kenya, ameongeza.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la mashirika yanayotoa huduma za bima inayoenda sambamba na sheria za Kiislamu maarufu kama Takafu.
Aidha kuna benki kadhaa sasa zinazotoa huduma za benki kwa mujibu wa sheria za Kiislamu nchini Kenya.
Kuenea huduma za kifedha za Kiislamu nchini Kenya na nchi zingine za Afrika ni ishara ya mwamko miongoni mwa Waislamu wa nchi hizo ambao wanataka maisha yao yaende kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
1070588