IQNA

Mfalme wa Saudia amwalika rais wa Iran katika kikao cha OIC Makka

14:17 - August 05, 2012
Habari ID: 2385582
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amemwalika Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran kuhudhuria kikao cha dharura cha Mshikamano wa Kiislamu kinachotazamiwa kufanyika tarehe 26-27 mwezi huu wa Ramadhani.
Ujumbe huo umewasilishwa na balozi wa Saudia nchini Iran Mohammad al Kilabi wakati alipokutana na Mkuu wa Ofisi ya Rais Rahim Mashai.
Balozi huyo amesema Mfalme Abdullah ameitisha ‘Kikao Kisicho cha Kawaida cha Mshikamano wa Kiislamu ili kuhakikisha kuna umoja katika kipindi hiki nyeti ambapo Waislamu wanakumbwa na mifarakano na fitina.’
Kikao hicho kinatazamiwa kujadili masuala muhimu yanayohusu umma wa Kiislamu. Imedokezwa kuwa kadhia ya Syria itatawala kikao hicho huku kukiwa na mashinikizo dhidi ya Damascus.
Waislamu wengi duniani wanaamini kuwa kadhia ya Palestina hasa kuukomboa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel ndio suala linalopaswa kupewa umuhimu na nchi za Kiislamu.
1071035
captcha