IQNA

Chuo cha Kikatoliki Ufilipino chapiga marufuku Hijab

22:55 - August 05, 2012
Habari ID: 2386257
Chuo kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki kusini mwa Ufilipino kimeibua utata baada ya kuwapiga marufuku wanafunzi wa kike Waislamu kuvaa Hijabu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mehol Sadai Mkuu wa Tume ya Kitaifa ya Waislamu Ufilipino Jumapili Agosti 5 amewatumia barua wakuu wa Chuo cha Pilar katika eneo la Zamboanga lenya idadi kubwa ya Waislamu akitaka uamuzi huo ubatilishwe.
Baraza la mji wa Zamboanga limekitaka chuo hicho kitafkari upya uamuzi huo. Inaaminika kuwa chuo hicho cha kikatoliki ndio cha kwanza kupiga marufuku Hijabu nchini Ufilipino.
Sadain amesema kuwa sera za kielimu nchini humo zinabainisha wazi kuwa wanafunzi Waislamu wa kike wana haki ya kuvaa Hijabu wakiwa katika shule na vyuo vya elimu na kwamba hawapaswi kulazimishwa kushiriki katika hafla zinazokinzana na Uislamu.
Karibu asilimia 80 ya watu milioni 100 Ufilipino ni Wakatoliki huku aghalabu ya waliosaliwa wakiwa ni Waislamu waishio kusini mwa nchi hiyo ya Asia.
1071625
captcha