Kwa mujibu wa Press TV, matamshi hayo yametolewa na Ali Iranpur mbunge wa eneo bunge la Mubarakeh katika bunge la Iran na kuongeza kuwa, kimya cha taasisi hizo kuhusu matukio ya nchi hizo ni jambo lisilokubalika kabisa. Amesema nchi za Magharibi zinaingilia masuala ya Syria kwa lengo la kugawa na kuwagonganisha Waislamu wa nchi hiyo.
Kuhusiana na suala la Myanmar ripoti za hivi karibuni zinabaini kwamba zaidi ya Waislamu 650 wameuawa kinyama na askari usalama pamoja na wanamgambo wanaungwa mkono na serikali na pia kupelekea maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kutokana na woga wa kuuliwa na magaidi wa Kibudha.
Serikali ya Myanmar imekataa rasmi kutambua haki za kimsingi za Waislamu wa nchi hiyo kwa hoja kuwa asili yao ni ya nchi nyingine. Hii ni katika hali ambayo historia ya nchi hiyo inapinga madai hayo yasiyo na msingi na kuthibitisha kwamba Waislamu waliingia nchini humo katika karne ya nane. 1074053