IQNA

Mshambuliaji wa msikiti wa Illinois Marekani aitiwa nguvuni

13:55 - August 14, 2012
Habari ID: 2392796
Polisi ya jimbo la Illinois nchini Marekani imetangaza kuwa imemtia nguvuni mtu aliye na umri wa miaka 51 kwa kushambulia kwa silaha msikiti wa Morton Grove katika jimbo la Illinois na kwamba uchunguzi kuhusiana na nia yake ya kufanya shambulio hilo ungali unaendelea.
Mhalifu huyo alifanya hujuma hiyo Agosti 11 baada ya swala ya Magharibi lakini kwa bahati nzuri hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa katika shambulio hilo la chuku dhidi ya Uislamu.
Ahmad Rahab, mkurugenzi mwandamizi wa Baraza la Uhusiano wa Uislamu la Marekani la jimboni Chicago amesema tukio hilo la kigaidi ni tahadhari muhimu kwa watawala wa Marekani kwamba hakuna usalama wa kutosha nchini humo na kuwa wanapasa kuchukua hatua za ziada ili kukabiliana na changamoto hiyo. Amesema silaha iliyotumiwa na mhalifu huyo ni hatari sana na kwamba ingemuua mara moja mlinzi mkuu aliyekuwa karibu na sehemu ya tukio hilo.
Ripoti zinasema kulikuwa na waumini 500 waliokuwa wakiswali kwenye msikiti huo wakati wa kufanyika shambulio hilo na kwamba mshambuliaji ama alikuwa na kusudio la kuogofya au kuua watu waliokuwemo humo.
Inasemekana kuwa mshambuiliaji huyo ni jirani wa msikiti huo ambaye mwanzoni alipinga vikali ujenzi wa msikiti katika eneo hilo. 1078414
captcha