IQNA

Hamas yawataka viongozi wa OIC kutetea Msikiti wa al Aqsa

16:04 - August 15, 2012
Habari ID: 2393971
Serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza imewataka viongozi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wanaokutaka mjini Makka kuchukua maamuzi ya kivitendo ya kukomboa Msikiti wa al Aqsa na Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya utawala ghasibu wa Israel.
Mshauri wa kisiasa wa Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina Yusuf Razqa amewaambia waandishi habari kwamba viongozi wa nchi za Kiislamu wanaokutana katika mji mtakatifu wa Makka wanapaswa kuitetea Quds Tukufu na Msikiti wa al Aqsa kwa kuchukua maamuzi ya kivitendo.
Amesema, kwa kawaida maamuzi yanayochukuliwa katika vikao kama hivi huishia kwenye maneno matupu na wala hayapewi umuhimu na utawala ghasibu wa Israel na madola makubwa ya Magharibi. Amesema inatarajiwa kuwa kikao cha sasa kitachukua maamuzi ya kivitendo.
Mshauri wa Ismail Hania amesema Wapalestina wanatarajia kwamba mabadiliko yaliyotokea kwenye nchi kadhaa za Kiarabu yatakuwa na taathira katika kuchukua maamuzi muhimu ya kuboresha hali ya Msikiti wa al Aqsa. 1079687

captcha