IQNA

Ayatullah Khamenei:

Jamhuri ya Kiislamu imeazimia haswa katika harakati za kufikia malengo yake

0:50 - September 02, 2012
Habari ID: 2402869
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi amekutana na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Jamhuri ya Watu wa Korea Kaskazini ambapo amazungumzia misimamo inayofanana ya pande hizo mbili katika masuala mengi na kusema: “Tunapaswa kuwa na azma kubwa katika harakati za kuelekea kwenye malengo yetu na wala tusiruhusu vikwazo na vitisho kuwa na taathira katika azma yetu.”
Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia kwelikweli katika harakati yake ya kuelekea kwenye malengo aali.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kuna nyanja nyingi za kupanua uhusiano wa nchi mbili hizi na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Korea Kaskazini zina maadui wa pamoja, kwa sababu madola ya kibeberu hayawezi kuzistahamili nchi huru na zinazojitawala.
Ayatullah Khamenei ameashiria safari yake nchini Korea Kaskazini wakati alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na kupongeza shakhsia ya kiongozi aliyeaga dunia wa nchi hiyo Kim Il Sung.
Katika maungumzo hayo Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Watu wa Korea Kaskazini Kim Yong-nam amewasilisha salamu za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Eun kwa Ayatullah Khamenei na kusema, safari ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Korea Kusini ilikuwa kipindi muhimu katika uhusiano wa nchi hizo mbili. Ameongeza kwamba moja ya siasa za kistratijia za Korea Kaskazini ni kupanua zaidi uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vilevile ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na maendeleo yake makubwa katika nyanja mbalimbali. 1089010
captcha