IQNA

Putin asisitiza juu ya nafai muhimu ya Uislamu nchini Russia

21:36 - September 03, 2012
Habari ID: 2404342
Rais Vladmir Putin wa Russia amesisitiza juu ya nafasi muhimu ya dini ya Uislamu nchini humo na kusema dini tukufu ya Uislamu imepata nafasi makhsusi kati ya raia wa Russia kutokana na thamani zake za kimaadili.
Rais wa Russia amesema katika ujumbe wake aliotoa kwa manasaba wa kutimia mwaka wa kumi tangu kuasisiwa Taasisi ya Hija ya nchi hiyo kwamba: “Hii leo dini tukufu ya Kiislamu inahesabiwa ni sehemu ya maisha ya kijamii na kiutamaduni ya Russia.” Ameongeza kuwa “Thamani za milele za Kiislamu zimejengeka kwenye masuala kama upendo, huruma na uadilifu, na mamilioni ya raia wa nchi yetu Russia ni wafuasi wa dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.”
Putin amemalizia kwa kusema kwamba, katika miaka ya hivi karibuni Taasisi ya Hija ya Russia imeimarika zaidi na kuchukua hatua za thamani katika kutatua masuala yanayohusiana na safari za Hija na kutuma misafara ya Waislamu wa nchi hiyo katika maeneo matakatifu ya kidini. 1089444


captcha