IQNA

UN yatahadharisha:

Gaza haitakuwa mahala pa kuishi hadi mwaka 2020

21:37 - September 03, 2012
Habari ID: 2404345
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa iwapo huduma za maji, umeme, afya na elimu hazitaboreshwa katika Ukanda wa Gaza huko Palestina eneo hilo halitakuwa sehemu ya kuishi hadi kufikia mwaka 2020.
Tovuti ya Muslim Village imemnukuu mratibu wa misuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Maxwell Gerald akisema kuwa hali ya maisha katika meneo la Ukanda wa Gaza kwa sasa ni ngumu na kwamba kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za kuboresha hali hiyo iwapo eneo hili linatakiwa kuwa sehemu ya kuishi mwanadamu.
Jamii ya watu wa Gazina ni watu milioni moja na laki sita na itafikia watu milioni 2.1 kufikia mwaka 2020; kwa msingi huo msongamano wa watu wakati huo utakuwa zaidi ya watu 5800 kwa kila kilomita mraba moja.
Sambamba na hayo miundombinu ya uzalishaji maji safi ya kunywa, umeme, huduma za kijamii na majitaka hitaoana na mahitaji ya uongezeko kubwa la idadi ya watu katika jamii.
Eneo la Gaza linazingirwa kikamilifu na utawala wa kidhalimu wa Israel tangu mwaka 2006 na linasumbuliwa na uhaba mkubwa wa nishati, dawa na ukosefu wa ajira ambao umefikia asilimia 45.
Umoja wa Mataifa umezitaka jumuiya za wahisani kuzidisha misaada yao kwa watu wa Ukanda wa Gaza wanaosumbuliwa na mzingiro wa pande zote wa utawala ghasibu wa Israel. 1089816
captcha