Kipindi cha "Uislamu, Kisa Ambacho Hakijasimuliwa" kilichorushwa hewani na Kanali ya 4 ya televisheni ya Uingereza na ambacho kimeendeshwa na mwanahistoria wa Chuo Kikuu cha Cambridge akiutaja Uislamu kuwa ni dini iliyobuniwa na wanadamu, kimezusha wimbi kubwa la malalamiko dhidi msomi huyo.
Ripoti zinasema kuwa mwanahistoria huyo wa Chuo Kikuu cha Cambridge amedai kuwa jina la mji wa Makka halikutajwa katika Qur'ani kuwa ndio kituo kikuu cha Uislamu kwa msingi huo Uislamu ni dini iliyobuniwa na wanadamu!
Baada ya kumalizika kipindi hicho raia Waislamu na wanahistoria waliwasilisha mashtaka yao dhidi ya mwanahistoria huyo kwa shirika linalosimamia vyombo vya habari nchini Uingereza wakilitaka kuchunguza matamshi ya mwendeshaji wa kipindi hicho yanayopotosha historia ya Uislamu. 1091177