IQNA

ISESCO yalaani maandamano dhidi ya Waislamu Myanmar

11:50 - September 08, 2012
Habari ID: 2407092
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limetoa taarifa likilaani vikali maandamano yaliyofanywa na Mabudha wa Myanmar wanaotaka kufukuzwa Waislamu nchini humo.
Taarifa la ISESCO imelaani vikali harakati za kupiga vita Uislamu nchini Myanmar na kutangaza kuwa, maandamano ya Mabudha na takwa lao la kufukuzwa Waislamu nchini humo ni mwendelezo wa mpango uliopendekezwa na viongozi wa serikali ya nchi hiyo.
ISESCO imesema, ukatili unaofanywa na viongozi wa dini ya Kibudha wa Myanmar unadhihirisha jinsi nchi hiyo inavyotumbukia katika kinamasi cha migawanyiko, siasa za misimamo ya kuchupa mipaka na ghasia ambavyo vyote vinasababisha ukiukwaji wa sheria za kimataifa na haki za binadamu.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo ISESCO imeutaka Umoja wa Mataifa, jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu, nchi zinazotetea amani na taasisi za Kiislamu kulaani vikali vitendo hivyo na kuchukua hatua za kuwalinda Waislamu nchini Myanmar.
Wiki hii makundi ya Wabudha wenye misimamo mikali yamekuwa yakifanya maandamano nchini Myanmar na kutoa wito wa kufukuzwa Waislamu nchini humo na kuchomwa moto misikiti yao. 1093463


captcha