Waandamanaji hao walishusha chini na kuchoma bendera ya Marekani huku wakiitaka serikali ya Cairo ikate uhusiano wake na Marekani.
Waandamanaji hao waliokuwa wamejawa na hasira walitoa nara za kutaka balozi wa Washington nchini Misri afukuzwe mara moja sambamba na kufungwa ubalozi huo. Aidha waandamanaji hao walitoa nara zisemazo, "Kwa roho na damu zetu tutajitoa mhanga kwa ajili ya Uislamu", "Marekani itaanguka" na "Allahu Akbar, Allahu Akbar" huku wakiitaja Marekani kuwa ni shetani mkubwa.
Wakati huo huo viongozi wa dini ya Kikristo nchini Misri wameungana na Waislamu katika maandamano hayo na kusisitiza kuwa, kitendo cha kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu kinalenga kuzusha fitina kati ya wafuasi wa dini hiyo na wale wadini nyengine hususan wenzao Wakristo. Mbali na viongozi hao wa Kikristo kulaani hatua ya kusambazwa kwa filamu hiyo, wameungana na taasisi 120 za Kikristo duniani katika kulaani hatua hiyo.
Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil leo ametangaza kuwa, nchi yake inalaani vikali filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na kusema kuwa, hatua hizo zinafanyika kwa lengo la kuzusha fitina kati ya Waislamu na wafuasi wa dini nyingine na kwamba njama hizo zitafeli. 1097192