IQNA

Iran yazidisha zawadi ya atakayemuua murtadi Salman Rushdie

19:34 - September 16, 2012
Habari ID: 2412837
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeongeza kiwango cha zawadi itakayotolewa kwa mtu atakay muua murtadi Salman Rushdie aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Kwa mujibu wa Ayatullah Sheikh Hassan Sane’ei anayesimamia Waqfu wa 15 Khordad, zawadi hiyo imeongezwa kwa dola laki tano na sasa imefika dola milioni tatu na laki tatu. Sheikh Sane’ei ametangaza habari ya kuongezwa zawadi hiyo wakati akitoa taarifa ya kulaani utengenezwaji filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW huko Mafrekani.
Itakumbukwa kuwa mwaka 1989, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini MA alitoa fatwa ya kuuawa murtadi Salman Rushdie alipochapisha kitabu chenye anwani ya Aya za Shetani "Satanic Verses" kinachomvunjia heshima Mtume SAW.
Ayatullah Sheikh Hassan Sane’ei amesema fatwa ya Imam Khomeini inalenga kukata mizizi ya njama za maajenti wa Marekani na Utawala wa Kizayuni. Amesema iwapo fatwa hiyo itatekelezwa maadui hawatathubutu tena kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu. 1099093

captcha