IQNA

Rais wa Misri ataka Umoja wa nchi za Kiislamu

22:55 - September 19, 2012
Habari ID: 2415520
Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema nafasi na mchango wa Iran katika kutatua matatizo ya Mashariki ya Kati ni mkubwa na wenye taathira chanya na kuongeza kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa na umoja na mshikamano kwa ajili ya kutimiza malengo yao.
Rais Muhammad Mursi wa Misri ameongeza kuwa nchi yake iko tayari kwa ajili ya kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kutafuta suluhisho la masuala ya Mashariki ya Kati.
Mursi ameyasema hayo Jumanne hii katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Cairo na kuongeza kuwa, Cairo iko tayari kushirkiana na Tehran na nchi nyingine za Kiislamu kutafuta suluhisho la matatizo ya eneo hili.
Amesema Misri na Iran ni nchi mbili kubwa zenye ustaarabu wa siku nyingi na kwamba hakuna tatizo lolote baina ya nchi hizo mbili
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasilisha salamu za taifa la Iran kwa Rais mpya wa Misri na akasema Jamhuri ya Kiislamu inaheshimu irada na matakwa ya watu wa Misri kwa ajili ya kushika hatamu za kujiamulia mambo yao wenyewe.
Vilevile amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kupanua zaidi ushirikiano wake na serikali ya Cairo.
1101861
captcha