Akihitubu mjini Tehran siku ya Ijumaa wakati wa kuanza 'Wiki ya Kujihami Kutakatifu' rais Ahmadinejad kwamba, waliojitoa muhanga kwenye vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran hawakuilinda nchi pekee bali pia heshima na utu wa mwanadamu.
Ameongeza kuwa, Iran ya Kiislamu imezidi kuwa imara siku baada ya siku na kuonya kwamba hujuma yoyote dhidi ya taifa hili itajibiwa kwa hasira na nguvu zote. Ndani ya wiki hii Iran itaonyesha mafanikio iliyopata katika sekta ya ulinzi pamoja na utayari wake wa kukabiliana na adui.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ijumaa imeanza wiki ya 'Kujihami Kutakatifu' ambapo ndani ya wiki hii taifa hili hukumbuka vita vya kulazimishwa kati yake na nchi jirani ya Iraq vilivyodumu kwa miaka minane.
Wairani wanakumbuka vile walivyolazimika kuilinda nchi yao dhidi ya uchokozi wa dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein aliyeivamia nchi hii Septemba 22 mwaka 1980.
1103270