IQNA

Iran yalaani vitendo vinavyomvunjia heshima Mtume

14:17 - September 22, 2012
Habari ID: 2416278
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kimya cha nchi za Magharibi mbele ya harakati za vyombo vyao vya habari zinazomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) ndio sababu ya kukaririwa vitendo hivyo viovu.
Ramin Mehmanparast amelaani uchapishaji wa vijikatuni vinavyomdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu nchini Ufaransa na kusema, kimya kinachofanyika kwa mpangilio maalumu katika nchi za Magharibi mbele ya mwenendo kama huo ni sehemu ya sera za kuuhujumu Uislamu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuchapishwa vijikatuni hivyo katika jarida la Kifaransa baada tu ya kuonyeshwa filamu inayomdhalilisha Mtume wa Uislamu huko Marekani ni njama iliyopangika kwa makusudi. Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaungana na Waislamu kote ulimwengu katika majonzi na maumivu hayo.

Amesema kuwa ushahidi unathibitisha kuwa duru za Wazayuni zimeshiriki katika kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa, Waislamu hawatavumilia vitendo viovu kama hivyo.

Katika kipindi cha sasa ambapo Waislamu kote duniani wanaandamana wakipinga filamu ya Kimarekani inayomtusi Mtume Muhammad (saw), jarida la kila wiki la Charlie Hebdola Ufaransa limechapisha vijikatuni vinavyomtusi na kumkejeli Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu.
1103280
captcha