IQNA

Kikao cha redio na televisheni za Kiislamu chaanza Tehran

14:54 - September 24, 2012
Habari ID: 2418075
Mkutano wa Baraza Kuu la Sita la Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu umeanza jana Jumapili kwa hotuba ya Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Shirika la Utangazaji la Irab mjini Tehran.
Mkutano huo unaofanyika chini ya kaulimbiu ya "Vyombo vya habari vya muqawama, mwamko wa Kiislamu hadi Kufikia Ushindi" unahudhuriwa na wawakilishi wa vyombo vya habari zaidi ya 280 kutoka nchi 35 katika mabara matano ya dunia.
Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Karimiyan Katibu Mkuu wa Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu amewasilisha ripoti kuhusu shughuli za Baraza Kuu la jumuiya hiyo.
Naye Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ambaye alikuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu katika mkutano huo ameeleza mitazamo yake kuhusu Mkutano wa Sita wa Baraza Kuu la Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu ulioanza leo hapa Tehran.
Moja kati ya ratiba za mkutano wa leo alasiri ilijumuisha uonyeshaji wa athari za tamasha zilizochaguliwa pamoja na filamu fupi fupi kuhusiana na mwamko wa Kiislamu. 1105064
captcha