IQNA

Wafilipino waandamana kulaani kutusiwa Mtume SAW

5:05 - September 25, 2012
Habari ID: 2418909
Mamia ya Wafilipino wameandamana nje ya Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila kulaani kutengenezwa filamu inayomvunjia heshima Mtume SAW huko Marekani.
Katika maandamano hayo ya Jumatatu, waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye maneno kama vile, 'Uhuru wa dini unatangulia uhuru wa maoni' na 'tunapinga undumakuwili wa Marekani'.
Waandamanji hao wameitaka serikali ya Marekani kupiga marufuku filamu hiyo chafu katika mtandao wa intaneti.
Aidha wamesema watawasilisha kesi katika Mahakama Kuu ya Ufilipino wakitaka filamu hiyo ipigwe marufuku nchini humo.
Maandamano ya kulaani filamu ya Kimarekani ya "Innocence of Muslims" inayomvunjia heshima Mtume saw yameendelea kushudiwa katika pembe mbalimbali duniani. Waislamu pia wanaendelea kulaani hatua ya gazeti la Charlie Hebdo ya kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume SAW.
1106067
captcha