IQNA

Mauaji ya vijana watatu wa Kishia Saudia yalaaniwa

15:57 - September 30, 2012
Habari ID: 2423069
Sheikh Abdul Hubail, mwanazuoni wa Kishia nchini Saudia amelaani vikali mauaji ya vijana watatu wa Kishia katika mji wa al Awamiya nchini humo.
Sheikh al-Hubeil ambaye ni Imam wa Msikiti wa Swala ya Ijumaa wa al-Abbas katika mji wa Rubeiiyya katika mkoa wa Qatif amesema kuwa kitendo cha askari usalama wa nchi hiyo cha kuwaua kwa risasi hai vijana watatu wa kishia wasio na hatia ni unyama mkubwa. Amesema inasikitisha kuona kwamba askari hao wanatumia mbinu za kuzusha hofu na woga miongoni mwa wanawake na watoto katika hali ambayo wanaweza kutumia zana za kisasa walizonazo kutuliza hali ya mambo katika maeneo ya Mashia bila kutumia nguvu za ziada.
Sheikh Abdul Hubail amesema umwagaji damu ya vijana hao utazidisha azma ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaodhulumiwa nchini humo kupigania haki zao za msingi kutoka kwa utawala dhalimu wa Aal Saud.
Vilevile ameashiria filamu ya Marekani inayomdhalilisha Mtume Mtukufu (saw) na radiamali dhaifu ya Rais Barack Obama iliyompelekea asichukue hatua yoyote ya kisheria dhidi ya wahalifu wa kitendo hicho cha dharau mbele ya vyombo vya sheria na kukumea vikali hatua ya rais huyo ambayo amesema imetokana na chuki yake dhidi ya Uislamu na Mtume Mtukufu (saw). 1110264
captcha