IQNA

Madai ya Bahrain dhidi ya Iran hayana msingi wowote

15:48 - October 01, 2012
Habari ID: 2423797
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kwamba, madai ya Bahrain kwamba, Tehran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo hili hayana msingi wowote.
Ramin Mehmanparast amekanusha vikali madai ya Khalid bin Ahmad bin Muhammad Aali Khalifa, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Bahrain aliyesema kwamba, Iran imekuwa ikifanya njama za kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Mashariki ya Kati.
Ramin Mehmanparast amesema kwamba, kukaririwa madai haya hakuna jipya na wala tuhuma kama hizi na mfano wake haziwezi kubadilisha uhakika na uhalisia wa mambo katika eneo hili. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amewataka viongozi wa Bahrain kusikiliza matakwa ya wananchi badala ya kutangatanga huku na huko wakizituhumu nchi nyingine.
1110816
captcha