IQNA

OIC yalaani mashambulizi ya mabomu Iraq

18:16 - October 01, 2012
Habari ID: 2423864
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya Iraq na kuua makumi ya watu wasiokuwa na hatia.
Ekmeleddin Ihsanoglu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu waliouawa katika mashambulizi hayo ya kigaidi na ameyataka makundi yote ya kisiasa ya Iraq kukomesha hitilafu zao na kutilia maanani maslahi ya kitaifa, usalama na umoja wa kitaifa.
Vilevile amewataka wananchi wa Iraq kuwa na subira na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuzusha machafuko kati ya makundi ya Kiiraqi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu pia ataelekea Ufaransa kesho na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo kuhusu hujuma inayofanywa dhidi ya Uislamu hususan hatua ya hivi karibuni ya jarida moja la nchi hiyo la kuchapisha vibonzo vinavyomdhalilisha Mtume Muhammad (saw). 1110872
captcha