Kwa mujibu wa tovuti ya OnIslam, Waislamu hao ambao walifanya maandamano ya amani katika mitaa ya miji tofauti ya nchi hiyo wamesema kuwa, wamefanya maandamano hayo ya amani kwa kuzingatia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu ambayo yanawataka kujiepusha na vitendo vya mabavu na ghasia.
Viongozi wa Waislamu wa India pia wameandaa vikao mbalimbali katika miji tofauti ya nchi hiyo ili kulaani na kukemea vitendo vya maadui wa Kiislamu vya kutengeneza filamu na kuchapisha vikatuni vinavyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na hasa Mtume Mtukufu (saw).
Wamesema Waislamu wanapasa kuimarisha umoja wao ili kuvunja njama zaidi za maadui dhidi ya matukufu yao. Wameviomba vyombo vya habari vya Kiislamu kuzidisha juhudi za kuarifisha sura halisi ya Uislamu na kutetea matukufu yake.
Waislamu wanaunda jamii ya watu milioni 160 kati ya watu wote bilioni 1.2 wa India. Nchi hiyo ndiyo iliyo na idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani baada ya Indonesia na Pakistan. 1112060