Kwa mara ya kwanza kabisa, Palestina imehudhuria kikao cha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kama mwanachama kamili.
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo, Palestina ilipata fahari hiyo mpya katika kikao kilichofanyika jana Jumatatu huko Muscat mji mkuu wa Oman na kuhudhuriwa na Irina Bokova, Katibu Mkuu wa UNESCO.
Shirika rasmi la habari la Palestina Wafa limesema ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadili mipango na bajeti ya UNESCO katika kipindi cha miaka ya 2014 hadi 2021.
Akizungumza katika kikao hicho Ismail at-Talawi, Katibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ya Palestina amezishukuru nchi zote za Kiarabu zilizofanya juhudi za kufanikisha Palestina ipate uanachama kamili katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa. 1112178