IQNA

Morocco yapiga marufuku kwa muda majarida ya Ulaya

16:02 - October 03, 2012
Habari ID: 2425330
Serikali ya Morocco imepiga marufuku kwa muda wa wiki moja usambazwaji nchini humo wa magazeti na majarida ya Ulaya kufuatia hatua ya majarida ya Hispania na Ufaransa ya kuchapisha vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Kwa mujibu wa tovuti ya Biladi, serikali ya Morocco imepiga marufuku kwa muda wa wiki moja uuzaji wa majarida sita ya Hispania na Ufaransa pamoja na gazeti moja la Ujerumani.
Akizungumzia suala hilo, Mustafa al-Khalafi, Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Morocco amesema kwamba wananchi wa nchi hiyo wamefurahia sana uamuzi huo wa serikali.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba majarida mawili ya Hispania na Ufaransa yalichapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume (saw) ili kunufaika kifedha, kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi yanazozikumba nchi za Ulaya. 1112508
captcha