Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Afrika, msikiti huo ulifunguliwa katika sherhee iliyofanyika saa kumi alasiri na kuhudhuriwa na Hujjatul Islam Mohammad Araqi mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS pamoja na idadi kubwa ya maulamaa, wasomi na Waislamu mjini humo.
Msikiti huo uliojengwa karibu na Chuo cha Kidini cha Imam Sadeq AS unatazamiwa kuwezesha Waislamu wa eneo hilo kushiriki katika vikao vya kieliumu kuhusu Uislamu na sayansi za Qur’ani mbali na kushiriki katika sala za jamaa.
Kigogo ni eneo lililo katika Wilaya ya Kinondoni mjini Dar-es-Salaam na wakaazi wa eneo hilo wanakadiriwa kuwa 40 elfu.
1111198