IQNA

Mashia wa Lebanon wapigwa marufuku kuingia Qatar

21:30 - October 06, 2012
Habari ID: 2426442
Watawala wa Qatar wamechukua hatua ya kushangaza na isiyo ya kibinadamu ya kupiga marufuku Mashia wa Lebanon kuingia nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Alam, Mashia wa Lebanon wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo vikubwa na kutendewa vitendo visivyo vya kibinadamu wanapoingia katika uwanja wa ndege wa Doha nchini Qatar.
Wanapoingia uwanjani hapo huzuiliwa katika vyumba maalumu na kukaguliwa mwili mzima na kisha kuulizwa maswali ya kukera kuhusiana na masuala ya kisiasa na vyama wanavyoviunga mkono.
Vilevile hukabiliwa na hali kama hiyo ya uchunguzi wanapoondoka nchini na kuonywa wasirudi tena nchini humo. Kwa kadiri kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Mashia wa Lebanon wapatao 11,000 wamezuiwa kuingia Qatar.
Watawala wa nchi hiyo wanadai kwamba hatua hiyo ya kinyama inatekelezwa kwa sababu za kiusalama. 1113571
captcha