IQNA

Waisraeli wachukizwa na Iphone 5

18:23 - October 08, 2012
Habari ID: 2428121
Waisraeli wa utawala ghasibu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamechukizwa mno na hatua ya kampuni ya simu ya Apple ya kutouonesha mji wa baitul Muqaddas (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel katika simu yake mpya aina ya Iphone 5.
Kituo cha Palestine Info kimeandika kuwa, gazeti la Kizayuni la Maariv limeripoti kuwa watumiaji wengi wa Kiisraeli wa simu ya Iphone 5 wanalalamika sana kutokana na kwamba ramani za simu mpya ya kampuni ya Apple haiutambui mji wa baitul Muqaddas kuwa ni mji mkuu wa Israel.
Gazeti hilo limeandika kuwa, watumiaji wa Iphone 5 wamegundua kwamba program za simu hiyo haziutambulishi mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) kuwa ni mji mkuu wa Israel japokuwa simu hiyo imezitaja nchi ngingine pamoja na miji mikuu yao.
Gazeti la Kizayuni la Maariv limeongeza kuwa program ya simu mpya ya Apple imeweka program mpya ya ramani badala ile ya Gogle Map na kuweka alama ya nyota katika miji mikuu ya nchi mbalimbali lakini haikuweka mji mkuu kwa ajili ya Israel.
Vilevile program ya wakati wa kimataifa ya simu ya Iphone 5 haiutambui mji wa Baitul Muqaddas kuwa ni mji mkuu wa Israel. 1115454


captcha