IQNA

Muafaka kati ya serikali ya Ufilipino na Waislamu

13:33 - October 09, 2012
Habari ID: 2428366
Serikali ya Ufilipino imefikia mwafaka na kundi kubwa kabisa nchini humo la wapiganaji wa Kiislamu la Moro Islamic Liberation Front (MLF) ambalo limekuwa likitaka kujitenga eneo la kusini mwa nchi hiyo.
Makubalino hayo na kundi la Moro Islamic Liberation Front (MILF), yanakusudia kuanzisha eneo la Waislamu lenye mamlaka ya ndani kusini mwa nchi linaloitwa Bangsamoro.
MILF imekaribisha uamuzi uliochukuliwa na Rais Benigno Aquino kumaliza mgogoro huo ulioanza miaka ya sabini na kupelekea karibu watu laki moja na nusu kupoteza maisha. Mpango huo wa amani unajumuisha makundi yote yaliyotaka kujitenga.
Lakini ukubwa wa eneo hilo jipya la Waislamu haujulikani na lazima mpango huo ukubaliwe kwa kura ya maoni ya wananchi ambao wengi wao ni Wakatoliki.
Nchi jirani ya Malaysia kupitia Waziri Mkuu Datuk Seri Najib Tun Razak imekuwa na nafasi muhimu katika kupatanisha pande hizo mbili.
1115757
captcha