IQNA

Wakristo wazidi kupungua Marekani

23:04 - October 10, 2012
Habari ID: 2429570
Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unaonesha kuwa idadi ya Wakristo wa Kiprotestanti imepungua na kufikia chini ya asimilia 50 ya watu wote wa jamii ya nchi hiyo.
Taasisi ya utafiti na uchunguzi wa maoni ya Pew imesema katika ripoti iliyopewa jina la 'Dini na Maisha ya Kijamii' kwamba mtu mmoja kati ya kila Wamarekani watano hujitambua kuwa mtu asiye na itikadi kwa dini yoyote.
Ripoti hiyo inasema kuwa kila mmoja kati ya vijana watatu wenye umri wa miaka chini ya 30 hujitambulisha kuwa hana dini makhsusi au anaamini baadhi ya masuala ya kidini na kiroho.
Taasisi ya utafiti wa maoni ya Pew imesisitiza kuwa, thuluthi moja ya vijana wa Kimarekani kutoka familia za Kikristo wameachana na Ukristo ilhaki kiwango hicho kati ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kimefikia asilimia 9.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa jamii ya Wakristo wa Kiprotestanti kuwa chini ya asilimia 50 na sasa imefikia asimia 48 ya jamii ya nchi hiyo. kupungua huko kwa jamii ya Wakristio wa kiprotenstai kumewatia wasiwasi mkubwa viongozi wa Marekani.
1117279
captcha