IQNA

Wamagharibi na Wazayuni wanaeneza vita Mashariki ya Kati

20:18 - October 12, 2012
Habari ID: 2429998
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Kazem Siddiqi amesema kuwa, Wamagharibi kwa kushirikiana na Wazayuni wanaeneza vita Mashariki ya Kati ili kudhoofisha harakati ya muqawama kwa ajili ya kuudhaminia usalama utawala haramu wa Israel.
Hujjatul-Islam Kazem Siddiqi ameyasema hayo katika hutuba za sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran. Akiashiria mivutano ya kimpaka na machafuko ya hivi karibuni kati ya Syria na Uturuki amesisitiza kuwa, Shirika la Kijeshi ya Nchi za Magharibi NATO na utawala wa Kizayuni wa Israel, zinafanya njama za kuitumbukiza Uturuki katika vita dhidi ya jirani yake Syria, kwa lengo la kuharibu usalama wa eneo hili sambamba na kudhoofisha muqawama kwa maslahi ya utawala ghasibu wa Israel. Aidha Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran ameashiria upinzani mkubwa wa hivi karibuni wa wananchi wa Uturuki kupinga hatua za aina yoyote ile za kijeshi za nchi yao dhidi ya taifa ndugu la Syria na kusema, viongozi wa Uturuki lazima wawe wavumilivu na kutatua matatizo yao na Syria kwa njia za kidiplomasia na kuepusha utumiwaji wa mabavu dhidi ya taifa jirani la Syria. Hujjatul-Islam Kazem Siddiqi ameashiria maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa kiimla wa ukoo wa kifalme wa Aal Khalifah na kusema, utawala ambao unafanya mauaji dhidi ya raia wake kwa kusaidiwa na askari wa Saudi Arabia na Wamagharibi, utawala wa aina hiyo hauna nafasi ya kuendelea kutawala na kwamba, hatimaye utashindwa tu na wananchi wenyewe wa Bahrain. Vile vile ameashiria vikwazo vya Wamagharibi vyenye lengo la kuzusha ghasia nchini Iran na njama za kuwagawa watu kikabila na na kimadhehebu nchini hapa na kulaani vikali hatua hizo alizozitaja kuwa zimeshindwa zamani. Hujjatul-Islam Wal Muslimina Kazem Siddiqi pia amesema, wananchi wa Iran mara zote wamekuwa wakishikama vilivyo kukabiliana na matatizo yanayowakabili na hivyo kuzishinda changamoto zote zinazojitokeza mbele yao.
1117317
captcha