IQNA

'Iran itasambaratisha njama zote za maadui '

22:38 - October 19, 2012
Habari ID: 2434107
Khatibu wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema, ulimwengu wa kibeberu unapaswa kutambua kwamba, taifa la Iran limestahamili magumu mengi na kwamba, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu litashinda njama na mipango yote ya maadui.
Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kubainisha kwamba, hatua ya madola ya kibeberu ya kushadidisha mashinikizo dhidi ya Iran na kutaka kuonyesha kwamba, hapa nchini kuna mgogogoro sambamba na hatua yao ya kueneza uzushi na uongo dhidi ya taifa hili ni baadhi ya mikakati ya maadui ya kukabiliana na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu hapa nchini. Ayatullah Khatami amewatahadharisha maadui wa mapinduzi ya Kiislamu akiwaambia kwamba, wanapaswa kutambua kwamba, hii leo taifa la Iran linahisi kuwa na nguvu na uwezo kuliko kipindi chochote kile. Ayatullah Khatami amesema, madola ya kibeberu yanataka kuonyesha kwamba, kushadidisha kwao vikwazo dhidi ya Iran kunatokana na Tehran kung'ang'ania kujipatia teknolojia ya nyuklia. Amesema, huu ni urongo wa wazi kwani katika kipindi cha miaka 30 iliyopita madola hayo yalikuwa yakiliwekea vikwazo taifa hili na wakati huo hakukuweko na dalili zozote za kutaka kujipatia teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.
1122228
captcha