IQNA

Iran yalaani uharamia wa Israel dhidi ya meli ya misaada Ghaza

11:06 - October 23, 2012
Habari ID: 2436504
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, hatua ya utawala wa haramu wa Israel ya kushambulia meli ya Kiswedeni iliyokuwa imebeba misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya wananchi wa Gaza huko Palestina ni ushahidi wa wazi wa uharamia wa baharani.
Ramin Mehmanparast amelaani hatua hiyo ya kinyama ya Israel na kusisitiza kwamba, uharamia huo wa Israel unakiuka wazi haki za binadamu. Mehmanparas amezitaka mahakama za kimataifa kuwafuatilia kisheria wale waliowateka nyara wafanyakazi wa meli ya misaada ya kibinadamu iliyokuwa ikielekea huko Gaza na kuchukuliwe hatua madhubuti na za kivitendo kwa minajili ya kukabiliana na dhulma za Wazayuni dhidi ya wananchi wanaokabiliwa na mzingiro wa huko Gaza, Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Itakumbukwa kuwa, siku ya Ijumaa vikosi vya majini vya Israel vilishambulia meli ya misaada ya kibinaadamu iliyotokea Ulaya ambayo ilikuwa imebeba misaada na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu kutoka nchi 30 duniani, na kuizuia kutia nanga katika Ukanda wa Gaza. Meli hiyo imepelekwa katika bandari inayodhibitiwa na Israel ya Ashdod.
1124108
captcha