IQNA

Sayyed Nasrallah amkosoa Obama kwa kuunga mkono Israel

9:52 - November 18, 2012
Habari ID: 2450111
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah ameikosoa Marekani kwa kuunga mkono bila masharti utawala wa Kizayuni wa Israel.
Amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel hauna budi ila kukubali haki za kisheria za Wapalestina.

Akizungumza mjini Beirut Jumamosi usiku, Nasrullah amesema Rais Barack Obama wa Marekani anaweza kusitisha hujuma za Israel huko Ghaza kwa kupiga simu mara moja tu lakini hafanyi hivyo. Kiongozi wa Hizbullah ameipongeza harakati ya Hamas kwa kufanikiwa kuvurumisha makombora katika mji wa Tel Aviv na ameuonya utawala wa Kizayuni kutothubutu kutekelelza hujuma ya nchi kavu dhidi ya Ghaza. Sayyid Hassan Nasrullah pia amezikosoa vikali nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa kushindwa kuchukua hatua za kivitendo kwa ajili ya kukomesha hujuma za Israel huko Ghaza.
1139227
captcha