IQNA

Udongo wa kaburi la Imam Hussein Karbala wabadilika na kuwa damu

19:50 - November 27, 2012
Habari ID: 2454740
Odongo wa kaburi la Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as) unaohifadhiwa katika jumba la makumbusho la Haram ya mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw) ulibadilika na kuwa damu katika siku ya Ashura yaani tarehe 10 Muharram ambayo ndiyo siku aliyouawa ndani yake.
Tukio hilo la kushangaza limeshuhudiwa na watu wengi wakiwemo viongozi wa kidini, wasomi na wahadhiri wa vyuo vikuu na kuakisiwa na kanali za televisheni.
Sayyid Hassan al Hakim ambaye ni miongoni mwa wahadhiri katika chuo kikuu cha kidini huko Iraq amesema tukio la kubadilika udongo huo wa kaburi la Imam Hussein unaohifadhiwa katika jumba la makumbusho la Haram ya Karbala ni taabiri ya dhulma na masaibu ya mjukuu wa Mtume (saw) Imam Hussein (as). 1143301
captcha