Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kwamba, kwa mujibu wa Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu, kuwatesa wanadamu ni kitendo kisicho cha kibinadamu lakini Marekani bila kuzingatia sheria za kimataifa ilizishambulia nchi kama Iraq na Afghanistan na kuwaua makumi ya maelfu ya raia wasio na hatia hasa wanawake na watoto na hivi sasa pia inawatesa maelfu ya watu katika jela za ndani na nje ya Marekani.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo Tehran pia ameashiria uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na makundi ya kigaidi nchini Syria na kusisitiza kuwa, Marekani kwa kuwapa magaidi silaha za kemikali inatekeleza jinai nyingine kubwa dhidi ya binadamu.
1153476