Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, mashinikizo na vitisho vinavyotolewa na Wamagharibi kamwe haviwezi kuwaondoa wananchi wa Iran katika mkondo wa ustawi na kufikia kwenye malengo na thamani za Mapinduzi ya Kiislamu.
Akielezea mfungamano wa wananchi wa Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na thamani za malengo ya mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Muhammad Ali Muwahedi Kermani amesisitiza kuwa, madola ya kibeberu yanapaswa kuelewa kwamba, wananchi wa Iran kwa kufuata miongozo sahihi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kamwe hawatarejea nyuma na kusalimu amri mbele ya njama na mashinikizo ya maadui. Khatibu wa sala ya Ijumaa ameongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanafuata harakati na nyayo za Imam Hussein AS kwani harakati hiyo ni taa ya kumwongoza mwanadamu kuelekea kwenye saada. Ayatullah Kermani amebainisha kuwa, nchi za Magharibi na hasa Marekani zinapaswa kuufahamu uhakika na kupata ibra kutokana na historia ya madikteta na madhalimu waliotangulia kwa kuacha kuwauwa wananchi wasio na hatia, na badala yake zifanye juhudi za kuleta amani na uthabiti duniani.