IQNA

Jarida la Ufaransa lamvunjia tena heshima Mtume (saw)

8:56 - January 06, 2013
Habari ID: 2475633
Jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo limechapisha kitabu kinachomvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW.
Jarida la vichekesho la Kifaransa la 'Charlie Hebdo' miezi michache iliyopita lilichapisha taswira inavyomvunjia heshima Mtume SAW na leo limechapisha kitabu cha vichekesho kilichopewa jina la 'Maisha ya Muhammad' ambacho kinazungumzia maisha ya Mtume Mtukufu Muhammad SAW.
Stephane Charbonnie Mhariri Mkuu wa jarida hilo linalotolewa kila wiki la Charlie Hebdo anadai kuwa, kitabu hicho kimetayarishwa kutokana na utafiti mkubwa uliofanywa na mmoja kati ya wataalamu wa elimu jamii Mfaransa mwenye asili ya Tunisia. Charbonnie amesema kuwa, alipata fikra ya kuandika kitabu hicho mwaka 2006, baada ya gazeti moja la nchini Denmark kuchora vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume SAW.
Jarida la Charlie Hebdo linalochapishwa kila wiki nchini Ufaransa, mwezi Septemba mwaka 2012 lilichapisha vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu SAW na kuamsha hasira za Waislamu kote duniani. 1165657
captcha