Sheikh Abdul Aziz Aal Sheikh ambaye ni mmoja wa maulama wa Kiwahabi nchini Saudia amewataka wananchi kutoa misaada yao ya kifedha kwa ajili ya makundi ya kigaidi ya Syria ambayo yanaendesha mauaji na kutega mabomu na hivyo kuua watu wasio na hatia.
Amesema kuwa, sasa sio jambo la busara kwa vijana wa Saudia kwenda na kushiriki katika vita dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad; lakini himaya ya kifedha kwa makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ndio njia bora kabisa. Wito huo wa Mufti Mkuu wa Saudi Arabia wa kutaka kusaidiwa magaidi wa Syria haujawashangaza sana walimwengu hasa kutokana na kuwa, tangu kuanza machafuko huko Syria serikali ya Saudia imekuwa ikiyasaidia wazi na pasina kificho makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya serikali ya Damascus. Weledi wa mambo wanazilaumu vikali Saudia, Qatar na Uturuki kwa kushirikiana na Marekani katika kuchochea machafuko nchini Syria sambamba na kuwapatia mafunzo, silaha na misaada ya kifedha waasi hao.
1167306