Waandamanaji hao waliokuwa na hasria wameelezea masikitiko yao kufuatia mauaji ya karibu Mashia 130 katika hujuma mbili za mabomu hivi karibuni huko Quetta na Bonde la Swat. Watu zaidi ya 300 pia walijireuhiwa katika hujuma hizo za kigaidi. Kundi la kigaidi la Lashkar-e-Jhangvi limekiri kutekeleza mauaji hayo ya kinyama. Maandamano ya kulaani ugaidi huo yamefanyika katika miji ya mikubwa ya Pakistan kama vile Islamabad, Karachi, Lahore, Quetta, Hyderabad, Sukkur, Khairpur, Multan, Muzaffarabad pamoja na miji mingine midogo ya nchi hiyo. Waandamanaji wamevilaumu vikosi vya usalama Pakistan kwa kushindwa kuwalinda Waislamu wa Kishia nchini humo. Aidha waandamanaji wameulaani vikali Ufalme Saudi Arabia kwa kuunga mkono makundi yenye misimamo mikali ambayo yanatekeleza hujuma za kigaidi dhidi ya Waislamu nchini Pakistan.
1170754