IQNA

Waislamu Tanzania watakiwa kujitegemea kiuchumi

20:18 - January 20, 2013
Habari ID: 2483415
Jumuiya ya Waislamu Mashia Tanzania (TIC) imefanya mkutano hivi karibuni katika mji mkuu wa Tanzania Dar es Salaam kwa lengo la kutambuana, kujuana na kufahamiana. Katika mkutano huo Waislamu wametakiwa kujitegemea kiuchumi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TIC kupitia tovuti ya ibn-tv.com
mkutano huo uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka takribani mikoa
yote ya Tanzania.
Kikao hicho cha siku mbili kilikuwa na mada kadhaa zilizowasilishwa
na masheikh kadhaa akiwemo Sayyid Aidarus kutoka Kenya ambaye
alizungumzia juu ya Uongozi, Sheikh Hemed Jalala ambaye aliongelea juu
ya Waislamu kuwa na tabia ya kukutana mara kwa mara, Sheikh Abdul
Razaq ambaye alizungumzia juu ya changamoto za Tabligh na walikuwepo
wataalamu wa masuala ya uchumi ambao nao kwa upande wao walihimiza
Waislamu kwa ujumla wao kuwa na tabia ya kujishughulisha ili
kujikwamua kiuchumi na badala yake wasiwe na tabia ya kuombaomba na
kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili.

Aidha, kwa upande wa wajumbe na wawakilishi wengine walipata nafasi ya
kuchangia na kutoa maoni na mapendekezo kulingana na mada
zilizowasilishwa pamoja na uhalisia wa Mashia jinsi wanavyoendesha
mambo ya kwa ujumla hapa nchini na kote ulimwenguni.

Mwisho viongozi pamoja na wajumbe waliondoka na azimio la kuwa na
tabia na mwenendo wa kukutana mara kwa mara ili kujuana na kufahamiana
sambamba na kuya tambua matatizo yao kwa ujumla.
1174462
captcha