IQNA

Rais Ahmadinejad: Mapinduzi ya Kiislamu ni harakati ya kihistoria

22:26 - February 10, 2013
Habari ID: 2494273
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo ameshiriki kwenye maandamano ya tarehe 22 Bahman yaani siku zinapofikia kileleni sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika uwanja wa Azadi yaani Uhuru, hapa mjini Tehran yaliyohudhuriwa pia na umati mkubwa wa wananchi, viongozi mbalimbali wa serikali na wanazuoni wa kidini, na kupongeza kuwadia mwaka wa 34 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Dakta Ahmadinejad ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ni harakati kwa ajili ya kufikia malengo ya Mwenyezi Mungu na ya kibinadamu. Amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ni harakati inayoendana na maumbile ya mwanadamu, na ndio maana mapinduzi hayo yanazidi kuimarika na kung'ara siku hadi siku. Amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran yameleta mwamko wa uhakika wa mambo na kumrejesha mwanadamu kwenye uhalisia wake. Dakta Ahmadinejad amesema, kwa kuyafikisha kwenye ushindi Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi wa Iran sasa wamekuwa ni walinzi na wasambazaji wa thamani za Mwenyezi Mungu. Vile vile ameashiria baadhi ya matunda na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, leo hii maadui wa taifa la Iran nao pia wanalikiri jambo hilo. Amesema madola yote ya uistikbari yameshindwa mbele ya azma thabiti ya wananchi wa Iran na kusisitiza kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ni kwa ajili pia ya kuhuisha izza na heshima ya taifa la Iran. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema, leo hii licha ya kuweko mashinikizo yasiyo ya kiinsafu ya maadui dhidi ya wananchi wa Iran, lakini serikali inafanya juhudi zake zote, usiku na mchana, ili kutatua matatizo ya wananchi.
1186238
captcha