Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour ameeleza kuwa, ushahidi uliotolewa na baadhi ya magaidi waliokamatwa umeonyesha kuwa, baadhi ya nchi za pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi na nchi jirani zinawafadhili kifedha na silaha magaidi na kuwashawishi watekeleze operesheni za kigaidi nchini Iran. Ameongeza kuwa, tangu mwezi Machi mwaka uliopita idadi kubwa ya makundi ya kigaidi yameingia nchini Iran lakini yamemakatwa na kusambaratishwa.
Hata hivyo Kamanda wa vikosi vya nchi kavu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hakutaja jina la nchi yoyote kuhusiana na kadhia hiyo.
1192114