Sergey Sobyanin amesema kuwa ofisi yake haitatoa tena vibali vya ujenzi wa misikiti mipya mjini Moscow kwa kisingizio kwamba Waislamu wanaotekeleza ibada za swala kwenye misikiti hiyo si raia wa Russia na kwamba ni rais wa kigeni wanaoishi nchini humo kwa ajili ya kazi.
Ameongeza kuwa asilimia 10 tu ya watu wanaotekeleza ibada za swala katika misikiti ya Moscow ni raia wa Russia na kwamba kuna misikiti ya kutosha kwa ajili ya idadi hiyo.
Meya wa Moscow ameongeza kuwa viongozi wa ngazi za juu wa mji wa Moacow hawaridhishwi na idadi kubwa ya wahajiri wanaoishi mjini humo na kwamba suala hilo lina madhara kwa mji huo.
Sergey Sobyanin amesema kuwa wakazi wa Moscow wanachukia kuona watu wenye lugha na mienendo tofauti katika mji huo.
Matamshi hayo ya meya wa Mosccow yamekosolewa sana na Waislamu wa Russia. Hii si mara ya kwanza kupigwa marufuku ujenzi wa misikiti jijini Moscow. Kwa sasa zaidi ya Waislamu milioni 23 wanaishi nchini Russia na inakadiriwa kuwa idadi ya Waislamu nchini humo itazidi watu milioni 50 hadi kufikia mwaka 2050. 1197076