IQNA

Miji Makka na Madina yashuhudia maandamano

5:45 - March 10, 2013
Habari ID: 2508710
Wananchi wa Saudi Arabia wamefanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Aal Saud katika miji mbalimbali ya nchi hiyo na kutaka Muhammad bin Nayef Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo ajiuzulu.
Taarifa zinasema kuwa, wananchi wa Saudi Arabia wamefanya maandamano katika miji ya Riyadh, Makka, Madina, Qatif na Baridah wakilalamikia kutiwa mbaroni na kuteswa wanawake nchini humo.
Hali kadhalika idadi kadhaa ya wanawake katika miji ya Makka na Madina wamefanya maandamano wakisisitiza juu ya kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa wale wote waliohusika na jinai za kuwanyanyasa, kuwatesa na kuwadhalilisha wanawake waliotiwa mbaroni.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, wiki iliyopita kikosi cha usalama cha Saudi Arabia kiliwatia mbaroni karibu watu 300 katika mji wa Baridah katikati ya nchi hiyo, wengi kati yao wakiwa wanawake na watoto.
1201229
captcha