IQNA

Hijabu yapigwa marufuku katika viwanja vya michezo Ufaransa

19:02 - March 20, 2013
Habari ID: 2513104
Binti mmoja wa Kifaransa aliyevalia vazi la stara la hijabu, amezuiliwa kujiandikisha kwenye somo la michezo kwa sababu eti amevaa vazi hilo la stara kwa mwanamke wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Kimataifa la Qurani (Iqna) limeandika kuwa, Nargese Bibimoune binti wa Kiislamu anayeishi katika mji wa Lyon nchini Ufaransa, amepigwa marufuku wakati alipokuwa akitaka kujiandikisha kwenye somo la michezo kwenye klabu moja iliyoko katika kitongoji cha Givors. Hii si mara ya kwanza kwa jamii ya wanawake wa Kiislamu nchini humo kukabiliwa na vitendo vya kibaguzi vinavyotekelezwa kwa misingi ya kidini. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Waislamu wamepigwa marufuku kuingia kwenye klabu moja ya michezo iliyoko katika eneo la Vigneux- sur-Seine kusini mwa jiji la Paris.
1206135
captcha