IQNA

Kiongozi Muadhamu katika mazungumzo yake na Rais wa Burundi:

Iran inakaribisha ustawi na umoja wa nchi za Kiafrika

21:18 - April 10, 2013
Habari ID: 2517638
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khameni mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliyeko safarini hapa nchini. Ayatullah Khamenei ameashiria mtazamo chanya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nchi za Kiafrika na kusisitiza kuwa, Iran inakaribisha ustawi na maendeleo ya nchi za Kiafrika na umoja miongoni mwao.
Amezungumzia hatua za kiadui za baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani za kuzikoloni nchi za Afrika na kuzusha njama na fitina katika nchi hizo na akasema: Nina matumaini kwamba nchi za Afrika ikiwemo Burundi, zitakuwa na mustakbali bora na maendeleo ya kudumu.
Amekaribisha suala la kustawishwa uhusiano wa Iran na Burundi na akasema kuwa, Umoja wa Afrika (AU) unaweza kuwa kituo madhubuti cha nchi zote za bara hilo, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono umoja na mshikamano katika jumuiya hiyo.
Kwa upande wake Rais Pierre Nkurunziza ameashiria uhusiano wa miaka 28 wa Iran na nchi yake na akasema lengo la safari yake mjini Tehran ni kuhuisha na kutia kasi mpya katika uhusiano wa nchi hizo mbili.
Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Rais Mahmoud Ahmadinejad, Rais wa Burundi ameashiria mashaka yaliyosababishwa na ukoloni barani Afrika na kusema kwamba, nchi za Afrika ikiwemo Burundi zinataka kuwa na mustakbali bora zaidi. 1211083

captcha