IQNA

Haram ya Sahaba wa Mtume Jafar Tayyar yachomwa moto

9:50 - May 05, 2013
Habari ID: 2528398
Siku mbili baada ya Mawahabi kuharibu kaburi la Sahaba wa Mtume (saw) Hujr bin Adi nchini Syria, wafusi wa kundi hilo nchini Jordan wamefanya maafa mengine na kuchoma moto Haram ya Swahaba Jafar bin Abi Twalib maarufu kwa jina la Jafar Tayyar, radhi za Mwenyenzi Mungu ziwe juu yake, huko kusini mwa nchi hiyo.
Mamia ya Mawahabi walivamia Haram ya Jafar Tayyar katika mkoa wa Karak na kulichoma moto.
Kaburi la Sahaba huyo mtukufu liko katika eneo la Mazar katika mkoa wa Karak na linaheshimiwa sana na Waislamu. Unyama huyo wa kuyavunjia heshima makaburi ya masahaba wa Mtume (saw) na mawalii wa Mwenyezi Mungu unaendelea kunyaziwa kimya na jumuiya na taasisi mashuhuri za Kiislamu zinazofandhiliwa au zenye uhusiano na utawala wa Saudi Arabia na waitifaki wake.
Sahaba Jafar Tayyar aliyekuwa kamanda wa jeshi la Kiislamu aliuawa shahidi katika vita vya Mauta baada ya kukatwa mikono miwili mwaka wa saba wa Hijra ya Mtume (saw). Baada ya kukatwa mikono na kufa shahidi Mtume (saw) alisema: Mwenyezi Mungu SW amempa Jafar mbawa mbili badala ya mikono yake ambazo anazitumia kupaa peponi.
Jafar bin Abi Twalib, ndugu yake Imam Ali bin Abi Twalib pia alikuwa kiongozi wa Waislamu waliohamia Uhabeshi wakikimbia adha na mauadhi ya washirikina wa Kiquraish. 1222234

captcha