IQNA

Rais Assad wa Syria awaonya magaidi na wafadhili wao

20:59 - May 24, 2013
Habari ID: 2537866
Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa serikali yake itaendeleza mapambano dhidi ya ugaidi na magaidi lakini pia itatumia njia za kisiasa kutatua mgogoro ulioikumba nchi hiyo.
Rais Assad amesema, magaidi wanaowaua raia wa kawaida watazidi kukabiliwa na mkono wa chuma na kwamba wafadhili wao wa kieneo na kimataifa nao hawatapewa nafasi ya kujitanua. Kiongozi huyo amesema hayo mjini Damascus alipoupokea ujumbe wa ngazi za juu wa serikali ya Tunisia. Rais Bashar al Assad amesema Damascus ina nia na irada thabiti ya kuona mgogoro ulioko nchini humo unatatuliwa kwa njia za kidiplomasia lakini pamoja na hayo serikali haiwezi kuwa mtazamaji tu wakati wananchi wasio na hatia wanauawa na kuhangaishwa. Hii ni katika hali ambayo, waasi wa Syria wamesema kuwa jana Alkhamisi walipokea shehena ya tani 35 za silaha kutoka kwa Saudi Arabia.
1232793
captcha