IQNA

Waislamu wa Myanmar wazuiwa kuzaa

12:35 - May 28, 2013
Habari ID: 2540112
Serikali ya Myanmar ikiwa na lengo la kuweka sheria za kibaguzi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo, imepitisha sheria ya ukomo wa kuzaa watoto wawili tu kwa Waislamu wa nchi hiyo.
Taarifa zinasema kuwa, sheria hiyo imepitishwa na kamisheni ya familia nchini humo. Kamisheni hiyo imeeleza kuwa sheria ya ukomo wa kuzaa watoto wawili tu imewekewa Waislamu tu na kwamba Mabudha wanaruhusiwa kuzaa zaidi ya idadi hiyo. Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali sheria hiyo na kusema kuwa inakiuka wazi haki za binadamu. Uamuzi huo wa serikali ya Myanmar umelaaniwa kimataifa.
Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu, Human Rights Watch limesema sheria hiyo ni ya kibaguzi.
Naye kiongozi wa upinzani Myanmar Aung San Suu Kyi pia ameitaja sheria hiyo kuwa ni ya kibaguzi na inayokiuka sheria.
Waislamu wa kabila ya Rohingya Myanmar wanakabiliwa na hali ngumu ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto nyumba zao, kunyanyaswa, kudhalilishwa na hata kuuawa, vitendo vinavyofanywa na Mabudda wenye misimamo ya kufurutu mipaka.
Serikali ya Myanmar nayo imeng'ang'ania msimamo wake ule ule kwamba, raia hao wa jamii ya Rohingya ni wahajiri wa Kibangladeshi na kwamba, sio raia wa Myanmar. Hadi sasa malefu ya Waislamu wa Rohingya wameuawa ikiwa ni natija ya vitendo vya kinyama dhidi yao vinavyofanywa na Mabudha nchini humo, huku maelfu ya wengine wakilazimika kuwa wakimbizi.
Licha ya jinai hizo kuendelea kufanywa mchana kweupe dhidi ya Waislamu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekataa hata kutuma tu kamati ya kuchunguza ukweli wa mambo nchini Myanmar, hatua ambayo kama ingefanyika bila shaka ingefichua zaidi dhulma, unyama na ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.
1234979
captcha