IQNA

Wairani watavunja njama za maadui katika uchaguzi

21:53 - May 31, 2013
Habari ID: 2541295
Khatibu wa sala ya Ijumaa amesema taifa la Iran kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa 11 wa rais litavunja njama za maadui wa mapinduzi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Sidiqqui Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameongeza kuwa kujitokeza kwa wingi wananchi katika uchaguzi kutakuwa na ujumbe wa kidini mbali na kuibua hamasa na izza isiyo na kifani ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sheikh Sidiqqui amesema kufanyika uchaguzi wa rais, mabaraza ya miji na vijiji Juni 14 kutakuwa ni ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameongeza katika kipindi cha miaka 33 iliyopita taifa la Iran limeonyesha ushujaa na umoja mbele ya maadui na kwamba hilo litashuhudiwa tena katika uchaguzi ujao. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameashiria kuwadia kumbukumbu ya kuaga dunia Imam Khomeini MA Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe nne Juni na kusema, ‘Imam MA alikuwa na imani kwa kura za wananchi na kwamba taifa la Iran kamwe haliwezi kupiga kura dhidi ya dini au kuwachagua watu mafisadi. Ameongeza kuwa Imam Khomeini MA aliarifisha Uislamu halisi katika maisha unaoenda kinyume na Uislamu bandia unaopigiwa debe na Marekani ambao ni Uislamu wa udhalilishaji.
1236480
captcha